Mdau wa Soka anaetambulika kwa jina @issambuzi_tz katika mtandao wa kijamii wa Instagram ameufungukiwa Uongozi wa Young Africans, baada ya kukubali kumuachia kirahisi Kocha wa kikosi cha wanawake klabuni hapo ‘Yanga Prinses’ Edna Lema.

Mwezi Juni Edna Lema aliomba kujiuzulu nafasi yake, na Uongozi wa Young Africans ulimkubalia ombi lake, na tayari nafasi yake imeshajazwa na Mchezaji wa zamani Mohamed Hussein ‘Mmachinga’.

Ni dhahiri @issambuzi_tz amekasirishwa na hatua hiyo na ndio maana akaamua kuufungukia uongozi wa klabu hiyo Kongwe katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram.

@issambuzi_tz ameandika: Kuna viongozi pale Yanga hawajui thamani ya hii timu inayoitwa Yanga Princess hawana mpango kabisa na timu ya wanawake.

“Wao wanataka iwe inashiriki tu, kikubwa isishuke daraja, ndiyo maana ishu ya Edna Lema kuandika barua ya kujiuzulu walichukulia powa tu na wakakubali haraka.

“Kwa sababu hawajui nini soka la wanawake. Yaani wapo viongozi hawajui hata mchezaji mmoja, na hata kwenda uwanjani kwao ni kitu kisichowezekana.

“Wasipobadilika kuanzia sasa timu itarudi kwenye kushika nafasi ya saba huko. Maana Simba na Fountain macho yote yapo pale na wanamwaga mpunga hasa.

“Kwa hii Spidi ya Fountain Gate Princess na Simba, wimbo unaenda kubadilika msimu ujao. Halafu aibu itabaki kuwa kwao.
“Wanajisahau sana, Edna alitakiwa kubakizwa kwa njia yoyote hata kama alikuwa na mapungufu yake.”

Chanjo ifike na vijijini - Naibu Waziri
Marufuku kuingia Uwanja wa Lake Tanganyika