Mshambuliaji kutoka nchini Burundi na klabu ya Young Africans, Fiston Abdul Razack, amefungasha kila kitu kilicho chake, kisha kutimka kambini.

Taarifa zinasema Mshambuliaji huyo aliyetua nchini kwa Mbwembwe wakati wa Dirisha Digo mwanzo mwa mwaka huu, ataondoka Dar es salaam na kurejea nchini kwao Burundi.

Fiston ambaye alisaini kandarasi ya miezi sita kuichezea Young Africans, mkataba wake huo umemalizika rasmi Jumatatu (Julai 12), hivyo amechukua uamuzi huo bila kushurutishwa.

Tangu ajiunge na Young Africans, Fiston amefunga mabao mawili katika michuano yote ambapo moja Ligi Kuu Bara na lingine Kombe la Shirikisho *ASFC*.

Barbara: Hatuna cha kujifunza kwa Young Africans
Muguna huyooo Azam FC