Afisa Mtedaji Mkuu wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC Barbara Gonzalez, amesema klabu hiyo haina cha kujifunza kwenye mchakato wa Mabadiliko wa Young Africans.

Barbara amesema hayo baada ya Wanachama wa Young Africans kupitisha kwa kauli moja mabadiliko ya katiba mwishoni mwa mwezi Juni, ambayo yatawaingiza kwenye mfumo wa uendeshajj mpya.

Kufuatia kuwepo kwa tetesi zinazodai kuwa Young Africans huenda ikapiga hatua kubwa itakapoingia rasmi kwenye mfumo huo mpya, tofauti na Simba SC, Barbara amesema haoni jambo ambalo litawateteresha kwenye utendaji.

“Sioni kama Simba SC ina kitu cha kujifunza kwenye mchakato wa Young Africans kwa sababu wao wanaanza wakati sisi tumemaliza,”

“Ni kama mwanafunzi aliyemaliza chuo na amefaulu awe na cha kujifunza kwa anayesoma form one, lakini sisi tunawatakia kila lakheri”

Mfumo mpya wa Mabdiliko ndani ya Young Africans unatoa nafasi kwa muwekezaji zaidi ya mmoja, tofauti na Simba SC yenye muwekezaji mmoja ambaye ni Bilionea Mohamed Ghulam Dewji ‘MO’.

Wazari Biteko atoa onyo STAMIGOLD
Fiston afungasha na kuondoka kambini