Uongozi wa klabu ya Azam FC umeendelea kutoa ufafanuzi wa suala la beki wao kutoka nchini Ghana Yakubu Mohamed, ambaye anahusishwa na mpango wa kusajiliwa na Young Africans.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesema taarifa zinazomuhusu beki huyo, sio za kweli na wanashangaa kwa nini zinaendelea kupewa nafasi kwenye mitandao ya kijamii.

“Kwanza sisi hatufuati sana habari za mitandaoni, na Young Africans bado hawajatuma ofa yoyote kwetu. Yakubu bado ni mchezaji wetu na ana mkataba, japo si mrefu sana, lakini hao wanaomhitaji au klabu yoyote kama inataka huduma yake tunawakaribisha tufanye biashara,” amesema Popat.

Kiongozi huyo amepinga dhana Azam FC huwa inaikatalia Young Africans inapotaka wachezaji kutoka kwao, akidai walishafanya biashara na Young Afrians kwa Gadiel Michael na Ditram Nchimbi.

“Hii dhana sio sahihi kabisa, kama biashara inatakiwa kufanyika tutaifanya, tumewahi kufanya hivyo kwa Gadiel Michael na Ditram Nchimbi ambao walitokea kwetu na kujiunga na Young Africans.”

Mkataba wa Azam FC na Yakubu unaisha Novemba 2021, hivyo Young Africans huenda wakatumia nafasi hiyo kuanza chochoko za kumsajili.
Kanuni za usajili zinatoa nafasi kwa klabu yoyote duniani kufanya mazungumzo na mchezaji aliesaliwa na mkataba wa miezi sita.

Tetesi za mchezaji huyo kutua Jangwani zinasema kuwa Young Africans imejipanga kumsajjli kwa mkataba wa miaka miwili.

Asukile amaliza atoka jela ya soka
Niyonzima: Naachana na Young Africans, Siachi mpira