Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ameagiza shamba la malisho ya mifugo lililopo Vikuge Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, kujiendesha kibiashara na kusambaza mbegu za malisho kutoka nchini China ijulikanayo kama JUNCAO maeneo mbalimbali nchini kwa kuwa ina sifa ya kustahimili sehemu yenye ukame ili wafugaji wapande malisho hayo.

Wakati akihitimisha ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo Naibu Waziri Ulega, amesema hayo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya shamba hilo na kumuagiza Katibu Mkuu anayeshugulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel kuhakikisha aina mpya ya malisho hayo inasambazwa na kusimamia vyema.

Amesema kuwa mbegu za malisho ya JUNCAO zisambazwe kuanzia ngazi ya mikoa wilaya hadi vijiji lengo likiwa kudhibiti mifugo na wafugaji kuhamahama kutafuta malisho huku akisisitiza kwenye mikoa ya ukame zaidi kama Dodoma, Singida, Manyara na Shinyanga.

“Mbegu hizi nataka zifike kwa haraka na kwa gharama nafuu ambayo kila mfugaji ataweza kununua aweze kuhudumia mifugo yake,” Amesema NAibu Waziri Ulega

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, akiwa ameambatana na Naibu Waziri Ulega ameomba malisho yanayozalishwa shambani hapo kuwanufaisha wakazi wa Mkoa wa Pwani.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ulega amekabidhi lambo la kunyweshea mifugo maji la Chamakweza lililopo Wilaya ya Chalinze Mkoani Pwani, huku akiiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Chalinze kuunda kamati kwa ajili ya kusimamia lambo hilo lililokarabatiwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Milioni 600 kwa ajili ya matumizi ya mifugo na binadamu.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega aliyechuchumaa akimpa maelezo Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete juu ya sifa za malisho ya mifugo yajulikanayo kama JUNCAO kutokea nchini China ambayo yamepandwa katika shamba la malisho ya mifugo lililopo Vikuge katika Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, ambapo Naibu waziri Ulega ametaka mbegu za malisho hayo zisambazwa kote nchini hususan vijijini
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Abdallah Ulega aliyechuchumaa akimpa maelezo Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete juu ya sifa za malisho ya mifugo yajulikanayo kama JUNCAO kutokea nchini China ambayo yamepandwa katika shamba la malisho ya mifugo lililopo Vikuge katika Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, ambapo Naibu Ulega ametaka mbegu za malisho hayo zisambazwa kote nchini hususan vijijini
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega (mwenye koti jeusi), akiangalia birika la kunyweshea mifugo maji wakati alipotembelea lambo kwa ajili ya matumizi ya mifugo na binadamu la Chamakweza lililopo Wilaya ya Chalinze Mkoani Pwani na kukabidhi rasmi lambo hilo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Chalinze kwa ajili ya matumizi ya wafugaji.
Muonekano wa sehemu ya lambo kwa ajili ya matumizi ya mifugo na binadamu ambalo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amelikabidhi kwa Halmashauri ya Manispaa ya Chalinze baada ya kukarabatiwa na serikali kwa zaidi ya Shilingi Milioni 600 na kuagiza kuundwa kwa kamati ya kusimamia lambo hilo.

Hatima ya Hausiboi aliyeua familia Dar
Watuhumiwa 71 wakamatwa Pwani