Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni Dar es Salaam limesema upelelezi kuhusu mauaji ya mama na watoto wake wawili wa kike umekamilika na faili limepelekwa Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali (DPP) kwa hatua zaidi.

Kamanda, Ramadhani Kingai amesema upelelezi umekamilika na jalada la kesi lipo kwa DPP, ambapo amesema kuwa Polisi walimkamata Shadrack Kapanga (34) akituhumiwa kufanya mauaji hayo akiwa ni mfanyakazi wa ndani katika familia hiyo.

Imefahamika kuwa Kapanga ni mtuhumiwa namba moja katika shauri hilo na pia polisi walimkamata aliyedaiwa kuwa alikuwa mpenzi wa Emily na hadi sasa wapo rumande.

“Jeshi la Polisi Kinondoni limeshakamilisha kazi ya uchunguzi wa sakata hili la mauaji na kwa upande wetu kama ilivyo kawaida tukishawasilisha faili kwa ofisi ya DPP tunangojea kama kunakuwa na maelekezo mengine,” amsema Kamanda Kingai.

“Kama likiwa sawa kwa maana ya upelelezi umekamilika inabakia suala la kupelekwa mahakamani kwa watuhumiwa na kuanza kwa kesi, kwa sasa bado tunawashikilia watuhumiwa hawa na wapo wawili aliyekuwa mfanyakazi na aliyekuwa mpenzi wa mama wa watoto wale waliouawa.”

Ilidaiwa kuwa Emilly Mutaboyerwa na binti zake Damita (13) na Daniela Mutaboyerwa (15), waliuawa Juni 9, mwaka huu na miili ilikutwa Juni 11 nyumbani kwao Mtaa wa Maryknol, Masaki wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.

Rwanda yatangaza marufuku ya kutotoka nje siku 10
Ulega ataka sekta ya Mifugo kujiendesha kibiashara