Mahakama Nchini Marekani imemuhukumu kifungo cha miezi 8gerezani Paul Hodgkins mwenye umri wa miaka 38 kwa kuhusika na uvamizi wa jengo la bunge na umwagaji damu mnamo Januari 6 katika nchi ya Marekani.
Mwendesha Mashtaka wa serikali Randolph Moss alibaini kuwa Hodgkins alifanya shambulizi kubwa kwa demokrasia, lakini kwa sababu alikiri kosa, alipunguziwa hukumu ya kifungo cha miezi 18 gerezani kilichopendekezwa na waendesha mashtaka.
Ambapo Hodgkins alihukumiwa kifungo cha miezi 8 gerezani na Mahakama, alishtakiwa kwa kuvamia jengo la bunge na kuzuia utendaji kazi wa wabunge.
Ilielezwa kuwa hukumu iliyotolewa kwa Hodgkins Florida inaweza kuwa kielelezo kwa takriban wafuasi 230 wa Rais wa Zamani wa Marekani Donald Trump ambao walizuiliwa kwa sababu ya uvamizi wa bunge mnamo Januari 6 na wanasubiri kuhukumiwa kwa shtaka moja.