Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Ilala kwa kushirikiana na Maafisa wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), maafisa uvuvi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na meneja wa Soko la Magogoni Feri wamekusanya samaki kiasi cha Kilogramu 164 waliokufa ufukwe wa karibu na Hospitali ya Agha Khan na Ocean Road.