Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo Agosti 3, 2021 akiwa ziarani nchini Rwanda amepata nafasi ya kutembelea baadhi ya uwekezaji wa viwanda nchini ikiwemo kiwanda cha kutengenezea magari CFAO MOTORS.
Aidha Rais Samia amemaliza ziara yake leo Agosti 3 iliyokuwa na lengo la kukuza uhusiano wa kimataifa na Nchi ya Rwanda hasa katika nyanja za uchumi na kibiashara, lakini pia marais hao wameshuhudia utiaji saini wa hati katika nyanja za uhamiaji, afya, elimu na TEHAMA.