Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo Agosti 3, 2021 akiwa ziarani nchini Rwanda amepata nafasi ya kutembelea baadhi ya uwekezaji wa viwanda nchini ikiwemo kiwanda cha kutengenezea magari  CFAO MOTORS.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame mara baada ya kuwasili katika eneo la Uwekezaji wa kiwanda cha Inyange Plant Entrance kilichopo mjini Kigali Rwanda leo tarehe 03 Agosti, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais Paul Kagame wa Rwanda wakitembelea katika kiwanda cha Inyange Plant Entrance mjini Kigali kinachozalisha Juisi, Maziwa na Maji ya kunywa leo tarehe 03 Agosti, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya aina ya simu zinazotengenezwa katika kiwanda cha Mara Phone Mjini Kigali Rwanda, wakati alipokua katika ziara yake ya siku ya pili nchini Rwanda leo tarehe 03 Agosti, 2021. Kulia ni Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakipata maelezo kutoka kwa Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha CFAO MOTORS kinachotengeneza Magari aina ya Vokswagen kuhusu huduma zinazotolewa wakati walipotembelea kiwanda hicho leo tarehe 03 Agosti, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakiwa mbele ya Gari aina ya Volkswagen mara baada ya kutembelea kwenye Kiwanda cha kutengenezea Magari CFAO MOTORS Mjini Kigali Nchini Rwanda leo tarehe 03 Agosti, 2021.

Aidha Rais Samia amemaliza ziara yake leo Agosti 3 iliyokuwa na lengo la kukuza uhusiano wa kimataifa na Nchi ya Rwanda hasa katika nyanja za uchumi na kibiashara, lakini pia marais hao wameshuhudia utiaji saini wa hati katika nyanja za uhamiaji, afya, elimu na TEHAMA.

Salula asaini miwili Azam FC
TANESCO yasisitiza utunzaji wa miundombinu