Siku moja baada ya Uongozi wa Kagera Sugar kutangaza kuwaacha wachezaji wanane, mmoja wa wachezaji hao Abdul-Swamad Kassim amefunguka ukweli wa safari yake ndani ya Simba SC.
Kiungo huyo kutoka visiwani Zanzibar amesema taarifa za kuhusishwa kwenda Simba SC zina ukweli, na tayari ameshamalizana na uongozi wa klabu hiyo inayoshikilia taji la Ligi kuu Tanzania Bara kwa mara ya nne mfululizo.
Kiungo huyo amesema amesaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Simba SC, baada ya kumaliza mkataba na klabu ya Kagera Sugar ambayo tayari imeshatangaza kuachana naye.
“Ni kweli nimesaini mkataba wa miaka mitatu na Simba SC, hatua hii ilikamilika baada ya kumaliza mkataba wangu na waajiri wangu wa zamani, Kagera Sugar, nimefurahi kutua Simba na niko tayari kwa ajili ya kuisaidia timu kufikia malengo yake.” amesema Abdul-Swamad Kassim
Wachezaji wengine waliaochwa Kagera Sugar ni Tinocco (keeper), Haroun Mussa (Beki), Hassan Isihaka(Beki), Ali Sonso (Beki), Mohammed IBRAHIM (Kiungo), Mussa Mossi (Kiungo), Abdulswamadu Kasim (Kiungo), Vitalis Mayanga (Mshambuliaji).