Kocha Mkuu Young Africans, Nasredine Nabi amesema kwa kiasi kikubwa uongozi wa klabu hiyo, umeifanyia kazi ripoti yake katika mapendekezo ya usajili kama vile ambavyo alikuwa anahitaji.

Nabi amesema awali mapendekezo yake ya kwanza alikuwa anataka beki mwingine wa kigeni na tayari kuna mmoja ambaye wameshamalizana nae ila bado kuja nchini tu na kutambulishwa.

Amesema baada ya hapo kuna maeneo mengine kama katika yamefanyiwa kazi kwa kuongezwa washambuliaji wawili, Fiston Mayele na Heritier Makambo ambao anaimani wataongeza makali ya nafasi hiyo.

“Ukiunganisha nguvu ya wale waliokuwepo msimu uliopita kama Yacouba Sogne mfungaji bora wa timu pamoja na Mayele, Makambo naimani kubwa tutakuwa na safu kali ya ushambuliaji yenye uwezo wa kufunga mabao mengi kuliko msimu huu,”

“Tumeimarisha safu yetu ya ulinzi kwa kusajili mabeki wa pembeni ambao naimani nao watakuja kuongeza uimara katika kuzuia na kuifanya timu yetu kutofungika kwa urahisi.”

Katika hatua nyingine Nabi amesema atakuwa na nafasi nzuri na uwanja mpana zaidi kuzungumzia usajili wa timu msimu huu na ripoti yake kiujumla pale dirisha litakapofungwa Agosti 31.

Nabi amesema bado kuna wachezaji wengine kama si watatu basi wawili ambao tutawasajili na baada ya hapo zoezi hili tutalifunga zaidi na wakati huo tutakuwa katika maandalizi rasmi ya msimu ujao.

Ni zamu ya Mlinda Lango Young Africans
Abdul-Swamad: Nimesaini Simba SC miaka mitatu