Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kufufua Vyuo vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu ili kuendelea kutoa mafunzo kwa kundi hilo maalum na kuhakikisha wanawezeshwa kupata ujuzi utakaowasaidia kujiajiri, kuajiri wenzao, kujiingizia kipato na kuchangia kwenye uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu Wenye Ulemavu Ummy Nderiananga, wakati akifungua Chuo cha Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu Luanzari Mkoani Tabora kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama kufuatia maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ya kutaka Vyuo vyote vya wenye Ulemavu kufunguliwa ifikapo mwaka 2025.

Amesema lengo la Serikali ya Awamu ya Sita ni kuhakikisha vyuo hivyo vinaendelea kutoa mafunzo kwa kuwajengea uwezo wa kujiendeleza vijana wenye ulemavu katika mazingira mazuri ya kujifunza ili waweze kujiajiri hatimaye kuondokana na maisha tegemezi.

“Ofisi ya Waziri Mkuu hivi karibuni ilifanya tathmini ili kujua hali halisi ya vyuo maalum vya ufundi stadi na huduma za utengamao hapa nchini kwa lengo la kubaini changamoto zilizopo na kuchukua hatua muhimu katika kuviwezesha vyuo hivyo kutekeleza majukumu yaliyokusudiwa,” Amesema Naibu Waziri Ummy.

Hata hivyo Naibu aziri Ummy amewahasa wadau mbalimbali kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita kwa kuchangia kufanikisha zozi hilo.

Sabaya na wenzake washtakiwa kwa makosa matatu
Kamwaga: Hatuchezi na Young Africans