Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imethibitisha kuwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili, Sylvester Nyegu pamoja na Daniel Mbura, wana kesi ya kujibu katika kesi ya jinai namba 105 ya mwaka 2021.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, amesema baada ya kusikiliza ushahidi wote uliotolewa na upande wa mashtaka, mahakama imebainika kuwa washtakiwa wote kwa pamoja wana kesi ya kujibu.

Hakimu Amworo anayesikiliza kesi hiyo amewaambia washtakiwa kwamba wanaruhusiwa kujitetea mahakamani hapo kwa njia ya kiapo au bila kiapo.

Aidha mahakama imewataka washtakiwa kutaja idadi ya mashahidi na vielelezo watakavyo kuwa navyo, na kwamba utetezi wao utaanza kusikilizwa hapo kesho.

Watuhumiwa hao wanashitakiwa kwa makosa matatu, ikiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha na wizi wa kutumia silaha ambapo kesi hiyo ilifunguliwa mahakamani hapo July 16 na kuanza kusikilizwa July 19 mwaka huu.

Tanzania yapanda viwango vya soka duniani
Serikali kufufua vyuo vya ufundi