Tanzania imeongeza pointi Sita kutoka 1088 mwezi Mei mwaka huu hadi 1094 mwezi huu Agosti, Tanzania imefanikiwa kupanda nafasi mbili kutoka 137 mwezi Mei hadi 135 mwezi huu katika Viwango vya Ubora wa Soka Ulimwenguni “FIFA Ranking” na nafasi ya 39 barani Afrika.
Afrika bado inaongoza na Senegal kwa muda sasa tangu mwaka jana, pia tunaendelea kushuhudia alama za Nigeria zikiendelea kushuka tu huku Cameroon na Ivory Coast wakiwa wanapandisha pointi zao taratibu taratibu.
Afrika Mashariki na kati, Uganda (84 duniani) wanazidi kuwa vinara, wanafuatia Kenya (104), Sudan (121), Rwanda (127) na Tanzania ndio inafuata 135.
Ethiopia (137), Burundi (140), Sudan Kusini (165), Djibouti (182), Somalia (196) na Eritrea wakiwa wa mwisho Duniani (204).