Wapinzani wa Young Africans kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Rivers United ya Nigeria, watashiriki michuano mifupi nchini Benin kwa ajili ya kujiandaa kimataifa.

Michuano hiyo maalum pia itashirikisha klabu nyingine za Afrika kama AS Vita ya DR Congo na Horoya AC ya Guinea.

Rivers United wamethibitisha kushiriki michuano hiyo ya Chalenji ya Afrika Magharibi, ambayo wanaamini itawasaidia kuikabili vilivyo Young Africans, kwenye hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwezi ujao.

Michuano hiyo imepangwa kuanza kesho Alhamisi (Agosti 19) mpaka Jumatano ijayo nchini Benin.

Timu zitakazoshiriki ni Hearts of Oak (Ghana), Union Sportive de la Gendarmerie Nationale (Niger), Arta Solar 7 (Djibouti), Loto-Popo FC (Benin), AS Vita Club (DR Congo) na AS Sonabel FC (Burkina Faso) na Les Buffles (Benin).

Kwa mantiki hiyo Rivers United imepiga hatua kubwa ya maandalizi tofauti na wapinzani wao Young Africans ambao jana Jumanne (Agosti 17) walianza kambi ya maandalizi nchini Morocco.

Hadi sasa Uongozi wa Young Africans haujathibitisha kama kikosi chao kitacheza mchezo wowote wa kimataifa wa kirafiki, zaidi ya kusubiri Siku ya Mwananchi ambapo imezoeleka hucheza mchezo wa kirafiki wa Kimataifa.

Bangala kutambulishwa Young Africans
ITC ya Aucho yakwama Misri