Klabu ya Young Africans imekamilisha usajili wa wachezaji wote kwenye mfumo wa usajili wa TMS wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) na Tanzania (TFF).

Mkurugenzi wa mashindano wa klabu hiyo Thabiti Kandoro, ambapo amesema usajili wa wachezaji wao wapya wameingia kwenye mfumo wa TMS msimu wa 2021-21.

“Tumekamilisha usajili wa wachezaji wetu wote 28, hii inamaanisha wote wameingia kwenye mfumo TMS wa CAF na TFF.”

“Pia tumeshapata ITC za wachezaji sita kati ya saba na tunaamini baada ya muda si mrefu tutapata ITC iliyobakia,”

“ITC iliyobaki ni ya Khalid Aucho kutoka klabu ya Misr Makassa ya nchini Misri ambapo tunataraji kuipata wakati wowote kuanzia sasa.” amesema Kandoro.

Young Africans tayari imeshaanza maandalizi ya msimu mpya kwa kuweka kambi nchini Morocco tangu jana Jumanne (Agosti 17).

Rivers United yaiandalia mkakati maalum Young Africans
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Augusti 18, 2021