Uongozi wa Young Africans ulioambatana na Kikosi nchini Mirocco, umesema kuna uwezekano wa kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki wakiwa nchini humo.
Young Africans imeweka kambi nchini Morocco, kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika 2021/22.
Makamu mwenyekiti wa kamati ya mashindano Young Africans Injinia Hersi Said amesema wamepokea maombi ya kucheza mchezo wa kirafiki.
Hersi amesema maombi hayo yamekuja kutoka kwenye klabu zaidi ya moja, lakini taarifa za ndani zinadai Raja Casablanca ndio wameomba kucheza na Mabingwa hao wa kihistoria Tanzania Bara.
“Suala la michzo ya kirafiki niseme tu Young Africans mpaka sasa tuna maombi ya klabu mbili za hapa (Morocco), zimeomba tucheze nao michezo ya kirafiki, hizo ni zile zenye uhakika na kwamba sisi tuamue,”
“Tumempelekea maombi hayo kwa kocha ataangalia sasa anahitaji kipi sisi hatuna cha kulazimisha.” amesena Hersi.
Young Africans itaanza kupambana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United Septemba 11 jijini Dar es salaam, kisha itacheza mchezo wa mkondo wa pili Septemba 18 nchini Nigeria.
Septemba 25 itapambana na Simba SC katika mchezo wa Ngao ya Hisani, Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijjni Dar es salaam.