Tanzania na India zimekubaliana kuweka msisitizo kwenye uwekezaji katika mnyororo wa uongezaji wa thamani wa madini,vitu vya thamani pamoja na mazao mbalimbali ikiwemo korosho ili kuuza bidhaa badala ya kuendelea na utamaduni wa kusafirisha malighafi.

Hayo yamejiri wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula, akipokea nakala za hati za utambulisho za Balozi Mteule wa India hapa nchini Binaya Srikanta Pradhan,

Ameongeza kuwa njia pekee kwa Tanzania kuongeza ajira na kupunguza umasikini ni kuwekeza katika mnyororo wa uongezaji wa thamani katika bidhaa za kilimo pamoja na madini.

Katika tukio jingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Misri hapa Nchini Mohamed Gaber Mohamed juu ya uwekezaji katika sekta ya uvuvi hususani uvuvi katika eneo la bahari lenye kina kirefu (deep sea fishing),viwanda vya nyama na sekta ya afya kwa kujenga hopitali kubwa Jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala ya hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa India Mhe.Binaya Srikanta Pradhan. Balozi Mteule Mhe. Binaya Srikanta Pradhan amekabidhi nakala za hati hizo katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Misri hapa Nchini Mhe.Mohamed Gaber Mohamed Abulwafa. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wametia msisitizo kuhusu uwekezaji katika mnyororo wa uongezaji wa thamani wa madini,vito vya thamani,uvuvi katika eneo la bahari la kina kirefu(deep sea fishing) afya,miundombinu pamoja na mifugo.

Bashungwa asisitiza wadau kushiriki kwenye marekebisho kanuni za utangazaji
Young Africans kutesti mitambo Morocco