Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa,  amewakaribisha wadau wa Sekta ya Habari nchini hasa wanaojihusisha na Huduma  za Utangazaji, masuala ya utoaji maudhui kwa Umma kupitia mitandao, redio na televisheni kutoa maoni katika Rasimu ya Marekebisho ya Kanuni za Maudhui  Mtandaoni za Mwaka 2020 pamoja na Kanuni za Maudhui ya Utangazaji katika  Redio na Televisheni za Mwaka 2018. 

Aidha marekebisho hayo yamefanywa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 165 cha Sheria ya Mawasiliano ya  Kielektroniki na Posta ya mwaka 2010, amesema Maboresho hayo yatazifanya Kanuni hizo ziendane na maendeleo ya teknolojia pamoja na kuongeza wigo wa upatikanaji wa  habari kwa wananchi. 

Rasimu za marekebisho ya Kanuni hizo zinapatikana kwenye tovuti ya Wizara  (www.habari.go.tz) pamoja na tovuti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania -TCRA (www.tcra.go.tz). 

Pia, Wizara inawakaribisha wadau wa huduma za utangazaji nchini kufika katika  mkutano wa wadau Agosti, 26, 2021, katika Ukumbi wa PSSSF (Zamani – LAPF)  Jijini Dodoma, kuanzia Saa 2.00 Asubuhi ili kuhitimisha zoezi la utoaji maoni. Wote  mnakaribishwa. 

TFNC, WFP wasaini mkataba wa milioni 595
Uwekezaji Tanzania, India kuimarika