Kikosi cha klabu ya KMC FC kimeanza rasmi kambi kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania Bara 2021/2022.

Klabu hiyo inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni ya Jijini Dar es Salaam, imeweka kambi Mkoani Morogoro ambapo itakuwa huko kwa maandalizi ya msimu mpya wa mwaka 2021/2022.

KMC FC iliondoka Jijini Dar es Salaam Jana Jumatano (Agosti 25) asubuhi na ilifika salama mkoani humo.

Ikiwa mkoani humo kwa maandalizi ya msimu mpya, KMC FC itakuwa na programu mbalimbali za mazoezi pamoja na kucheza michezo ya kirafiki kama program inavyoonyesha kwa lengo la kuwapima na kuwaweka vizuri wachezaji kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu itakayoanza Septemba 27 mwaka huu.

Aidha kuhusu suala la usajili, Klabu hiyo inaendelea kufanya usajili na wakati wowote kwa utaratibu wa klabu utakapokamilika itaanza kuwatambulisha wachezaji wote ambao wamesajiliwa katika dirisha kubwa lililofunguliwa mapema mwezi huu Agosti.

Hata hivyo KMC FC imewafahamisha mashabiki, wapenzi na Watanzania kwa ujumla kuwa usajili unaoendelea kufanyika umezingatia matakwa ya Bnchi la Ufundi na inasajili wachezaji wenye viwango vya hali ya juu na bora watakaoleta manufaa makubwa katika Timu yetu.

Imetolewa leo Agosti 26
Na Christina Mwagala
Afisa Habari na Mahusiano KMC FC

Mo Dewji ampotezea Haji Manara
Manara aishambulia tena Simba SC