Wakati Mwanafamilia Mpya wa Young Africans Haji Manara akipigilia Misumari kwa kusema yanayoihusu klabu ya Simba SC, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu Bingwa Tanzania Bara Mohamed Dewji ‘Mo’ amempotezea na kuweka mambo ya kimaendeleo kwenye kurasa zake za Mitandao ya kijamii.

Haji Manara mapema hii leo alihojiwa kwenye kipindi cha Sports Arena cha Wasafi FM na kuzungumza mambo mengi yanayohusu Simba SC, huku akihoji Shilingi bilioni 20, ambazo zilikabidhiwa na Mwenyekiti huyo kwa Uongozi wa klabu hiyo siku chache, baada ya kuondoka klabuni hapo kama Msemaji.

Katika hali mshangao ‘Mo’ hajajibu lolote kuhusu tuhuma alizorushiwa na Haji Manar, badala yake ameweka picha akiwa nchini Marekani aliyoipa maelezo yanayosomeka kuwa: Ilikua ni furaha kukutana na Jason Levien, ambae ni mmiliki wa klabu ya mpira wa miguu ya DC United ambayo ina thamani ya dola za kimarekani millioni 700! @dcunited
Nina furaha kutangaza ushirikiano mpya kati ya klabu za DC United na Simba.


Ifikapo mwaka 2022, klabu ya Simba itasafiri kwenda Marekani kwaajili ya mazoezi na maandalizi ya msimu mpya, na pia itashiriki katika mashindanobya kimataifa yatakayoandaliwa na klabu ya DC United, ambayo yatahusisha ligi ya MLS na vilabu kutoka Amerika ya Kusini.

Akutwa akifanya tendo la ndoa na mwanafunzi wa darasa la nne
KMC FC yajichimbia Morogoro