Meneja wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC, Patrick Rweyemamu amesema msafara wa watu 34 (wachezaji 23 na viongozi 11) wataondoka leo jijini Dar kuelekea Arusha kwa ajili ya kambi ya majuma mawili ya maandalizi ya msimu ujao (2021/22).
Rweyemamu amesema kuwa kwenye wachezaji 23 wamejumuishwa na wachezaji kikosi cha wachezaji wa U20 na ambao wapo timu za Taifa watajiunga na kambi jijini Arusha watakapomaliza majukumu yao kwenye timu za taifa.
Wachezaji wa kikosi cha wakubwa ambao wanatarajia kuondoka leo upande wa Walinda Lango ni Ally Salim, Beno Kakolanya na Jeremiah Kisubi.
Mabeki ni Gadiel Michael, Joash Onyango, Hernock Baka Varane, Pascal Wawa
Viungo: Jonas Mkude, Sadio Kanoute, Hassan Dilunga, Abdulswamad Kassim na Rally Bwalya.
Viungo Washambuliaju (Mawinga): Benard Morrison, Ousmane Sakho, Jimmyson Mwinuke, Yusuph Mhilu na Duncan Nyoni
Washambuliaji: Ibrahim Ajibu, Chris Mugalu na Kibu Dennis.