Afisa habari na msemaji wa zamani wa Yanga, Jerry C. Muro, ambaye sasa ni mkuu wa wilaya ya ikungi mkoani Singida, amesema kwa sasa amejikita katika kulihudumia taifa kwa ujumla wake badala ya kupitia nyanja moja pekee, kama michezo.

Akiwa katika ziara ya kikazi ya kutatua kero na changamoto za wananchi wa kijiji cha Ighuka kata ya Ikungi, Muro amesema anajua mpira unamhitaji na watu wamemmisi, lakini kwa sasa hana mawazo ya kurudi kwenye mpira.

“Kama ni kufanya kitu kwa ajili ya mpira, basi nitafanya katika wilaya yangu ya Ikungi kwa sababu kuna vijana wengi wana vipaji na pia kuna timu nyingi na mashabiki wengi”.

Muro amesema hata yeye amesikia tetesi za baadhi ya vilabu vikubwa kumfikiria kuwa msemaji ili kuchangamsha mpira ambao kama alivyofanya zamani.

“Unajua tangu niondoke kwenye mpira, hakuna tena mtu wa kuunguruma hadi nchi ikatikisika.

Mimi niliita watu airport pale wakajaa…hawa mnaowaona sasa kujaa airport kupokea wacheaji, ni zao la mbegu niliyopanda mimi”.

Simba SC kuingia kambini Arusha leo
Mdhamini wa Ligi Kuu kutangazwa mwezi huu