Imebainika kuwa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC imewasilisha majina ya wachezaji 31 waliosajiliwa kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu wa 2021/22.

Simba itakayoiwakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo imepeleka idadi kubwa ya wachezaji waliosajiliwa CAF kwa mara ya kwanza tangu ilipoanza kushiriki michuano hiyo.

Kwa upande wa Young Africans imebainika kuwa, wamewasilisha orodha ya wachezaji 28 waliowasajili kwa ajili ya michuano ya Afrika.

Wachezaji wa Simba waliosajiliwa kwa ajili ya michuano ya Afrika, upande wa walinda lango wapo wanne (4) ambao ni Aishi Manula, Benno Kakolanya, Jeremiah Kisubi na Ally Salim katika

Mabeki wapo tisa (9): Erasto Nyoni, Mohammed Hussein, Gadiel Michael, Henock Inonga ‘Varane’, Israel Mwenda, Joash Onyango, Pascal Wawa, Kennedy Juma na Shomari Kapombe

Viungo wapo kumi na tatu (13): Abdulswamad Kassim, Bernard Morrison, Duncan Nyoni, Hassan Dilunga, Jimmyson Mwanuke, Jonas Mkude
Mzamiru Yassin, Pape Ousmane Sakho, Peter Banda, Rally Bwalya, Sadio Kanoute, Thadeo Lwanga na Ibrahim Ajibu

Washambuliaji wapo watano (5): John Bocco, Meddie Kagere, Chriss Mugalu, Yusuph Mhilu na
Kibu Denis.

Waziri Gwajima azindua kliniki tembezi za magonjwa ya TB
CCM yatoa maelekezo matatu kwa serikali