Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa rai kwa wazalishaji na watengenezaji wa matofali ya mchanga na saruji kuhakikisha wanazalisha matofali yenye viwango vinavyotakiwa ili kuweza kumlinda mtumiaji asiweze kupata madhara.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 8, 2021 Jijini Dar es Salaam Afisa Viwango Idara ya Uandaaji wa Viwango TBS, Azizi Msemo amesema kuwepo kwa viwango vya matofali itawasaidia pia wazalishaji wa matofali watakapokuwa wamethibitisha ubora watakuwa na uhakika hata wakupata masoko kuuza bidhaa zao ndani na nje ya nchi.
Akielezea kuhusiana na dhumuni la TBS kuandaa viwango vya matofali amesema kuwa kwa kufanya hivyo itasaidia kulinda usalama wa wananchi tofauti na jengo likijengwa na matofali yenye viwango vya chini maafa yakitokea kama vile tetemeko au mtikisiko inaweza kusabisha madhara ya kwa wananchi hao.
“Unaponunua bidhaa ambayo haina ubora ukiitumia leo na kuharibika utahitaji kununua nyingine kwahiyo utakuwa haujazingatia suala lla uchumi hivyohivyo kwa upande wa matofali pale unapojenga jengo ambalo matofali yake hayana ubora unaotakiwa basi utahitajika kufanya matengenezo ya mara kwa mara wa hilo jengo,” Amesema Afisa Msemo.
Amesema Shirika la Viwango TBS wana kiwango no.TZS283 ambacho kinaianisha matakwa ya matofali ambayo yanatengenezwa kwa simenti na mchanga ili kuweza kuhakikisha mtumiaji asiweze kupata madhara.