Wakili wa Kampuni ya Tigo Fred Kapala amesema kampuni hiyo huweka kipaumbele katika kutii sheria za mamlaka kuliko siri za wateja.
Kapala ameyasema hayo Leo Novemba 3 mbele ya Mahakama ya makosa ya Uhujumu uchumi ambapo alikua shahidi katika kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.
Baada ya kusema hayo taarifa hiyo imezua taharuki kwa wateja wengi wa mitandao ya simu ambapo wamehoji juu ya Umuhimu wa Tanzania kuwa na Sheria na ulinzi wa taarifa binafsi za wananchi ili kuhakikisha Ulinzi, Usiri na Usalama wa faragha zao.
Kukosekana kwa Sheria hiyo kumekua kukipelekea kuuzwa au kutolewa kwa taarifa binfasi za wateja kwa mamlaka za Serikali au Makampuni bila idhini ya Mteja.