Mahakama Nchini Sudani imeamuru kurejeshwa kwa huduma za Intaneti zilizokatwa wakati wa Mapinduzi ya Kijeshi kwa zaidi ya wiki mbili zilizopita.

Kwa mijibu wa Wakili Abdul-Azim Hassan wakati akizungumza na Shirika la Habari la AFP amesema kuwa Mahakama ya Wilaya mjini Khatum imeamuru huduma za Intaneti kurejeshwa mara moja.

Hata baada ya agizo la Mahakama Nchi hiyo imesalia bila Intaneti, mapema siku ya Jumanne kesi hiyo ilifunguliwa na Kundi la Wanasheria na Jumuiya ya Ulinzi wa Wateja wa Sudan

Upatikanaji wa Intaneti Nchini Sudan kwa kiasi kikubwa ulizuiwa tangu Oktoba 25 yalipofanyika Mapinduzi ya Kijeshi huku Mawasiliano ya Simu pia yakitatizika mara kwa mara.

Jeneral Mkuu wa Sudani Abdel Fattah al-Burhan aliivunja serikali na kutangaza hali ya hatari na kuuweka kizuizini uongozi wa kiraia.

Waziri Mkuu Abdalla Hamdok alikamatwa na kisha kuweka chini ya kizuizi cha nyumbani.

Itakumbukwa siku moja kabla ya mapinduzi Burhan alivishutumu vyombo vya habari vya mtandaoni kwa kuzusha uchochezi lakini pia aliahidi kwamba huduma za mtandao zitarejea taratibu.

Idadi kubwa ya wanaharakati wanaounga mkono demokrasia wamekatwa tangu kutokee mapinduzi ambayo yalisababisha maandamano ya nchi nzima na ukandamizaji ulisababisha vifo vya watu takribaki 14 kutokana na ripoti ya madaktari.

Uwanja wa Jamhuri Dodoma waboreshwa
Kocha Pablo ndani ya Bongo