Kocha Mkuu Mpya wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Pablo Franco Martin amewasili jijini Dar es salaam tayari kwa kuanza kazi ya kukinoa kikosi chake.

Kocha Pabro Raia kutoka nchini Hispania aliwasili Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mapema asubuhi na kupokelea na Mratibu wa Simba SC Abbas Ally.

Baada ya kuwasili kocha huyo ameonyesha kufurahia mazingira ya Dar es salaam kufuatia uso wake kuwa na bashasha, huku Wadau wa soka Uwanjani hao wakimlaki na kumkaribisha nchini.

“Karibu tanzania Kocha, tulikua tunakusubiri kwa hamu kubwa, tunakutakia kazi nzuri na yenye mafanikiuo kocha.” Walisika baadhi ya Mashabiki waliokuwepo uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.

Kabla ya kuanza safari ya kuja Dar es salaam-Tanzania Kocha Franco Pablo Martin alituma salamu kwa Mashabiki wa soka wa Simba SC kwa njia ya Video huku akisema: “Nimefurahishwa kwenda Tanzania kujiunga na klabu ya Simba SC Tanzania, Simba ni moja klabu kubwa barani Afrika yenye mashabiki bora sana, ninatumaini tutaonana hivi karibuni, Nguvu moja” amesema Kocha Franco kupitia Simba App.

Simba SC ilifungua Dirisha la kusaka Kocha Mpya baada ya kuachana na Didier Gomes mwishoni mwa mwezi Oktoba, kufuatia kocha huyo kutoka nchini Ufaransa kushindwa kufikia malengo ya klabu hiyo kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Simba Ilikwama kwenye Michuano hiyo, kufuatia kufungwa maboa 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salam, huku ikitangulia kushinda ugenini mjini Gaborone mabao 2-0.

Intanenti yarudishwa baada ya kuzimwa kwa wiki mbili
Rais Samia aelekea nchini Misri kwa ziara ya siku 3