Kocha Mpya wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Franco Pablo Martin ameendelea kufunguka, baada ya kutangazwa kushinda nafasi ya kuwa Mkuu wa Benchi la Ufundi la klabu hiyo.

Kocha Franco alitangazwa kuwa Kocha Mkuu Mpya wa Simba SC Jumamosi (Novemba 06) majira ya usiku, baada ya kutimiza vigezo vilivyowekwa na Uongozi wa klabu hiyo kupitia mchakato ulioendeshwa kwa zaidi ya juma moja.

Kocha huyo kutoka nchini Hispania amesema amefurahia kupata kazi nchini Tanzania, tena katika klabu ya Simba SC ambayo inashirikiki Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Amesema Simba SC ni moja ya klabu kubwa Barani Afrika, yenye Mashabiki bora sana, huku akiwahidi kuona nao hivi karibuni, baada ya kuwasili jijini Dar es salaam.

“Nimefurahishwa kwenda Tanzania kujiunga na klabu ya Simba SC Tanzania, Simba ni moja klabu kubwa barani Afrika yenye mashabiki bora sana, ninatumaini tutaonana hivi karibuni, Nguvu moja” amesema Kocha Franco kupitia Simba App.

Simba SC ilifungua Dirisha la kusaka Kocha Mpya baada ya kuachana na Didier Gomes mwishoni mwa mwezo Oktoba, kufuatia kocha huyo kutoka nchini Ufaransa kushindwa kufikia malengo ya klabu hiyo kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Simba Ilikwama kwenye Michuano hiyo, kufuatia kufungwa maboa 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salam, huku ikitangulia kushinda ugenini mjini Gaborone mabao 2-0.

Sekta ya Madini yazidi kuneemeka kiuwekezaji
Coastal Union yaalani Fair Competition