Uongozi wa Azam FC upo kwenye mawindo ya Usajili wa wachezaji watatu kupitia dirisha dogo la usajili ambalo litafunguliwa rasmi mwezi ujao.

Azam FC imeanza vibaya msimu huu 2021/22, hali ambayo imewaamsha viongozi wa klabu hiyo kuingia kwenye mpango wa kukiongezea nguvu kikosi chao chini ya usaidizi wa Kocha George Lwandamina.

Mpango kazi unatajwa kuchorwa kwa kuwafuata nyota kutoka nchini Rwanda kwa lengo la kuboresha kikosi hicho ambacho kimeanza kwa kasi ya upole ndani ya Ligi Kuu Bara.

Eneo la ushambuliaji la klabu hiyo limeonakana kupoa kwa kuwa kwenye michezo mitano ambazo ni dakika 450 safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao manne huku bao moja likifungwa na beki ambaye ni Daniel Amoah.

Habari zinaeleza kuwa bado muunganiko wa washambuliaji wapya unampa tabu Idd Seleman ‘Nado’ ambaye alikuwa na ukaribu mkubwa na Prince Dube ambaye kwa sasa ni majeruhi.

Mmoja wa mabosi wa Azam FC ameweka wazi kuwa Azam FC inatafuta kiungo mmoja matata sana,beki wa kazi chafu pamoja na mshambuliaji wa kufunga mabao kila mchezo.

Yacouba Sogne apelekwa Tunisia
Hitimana afunguka kumuweka benchi Wawa