Kikosi cha Azam FC kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU SC ya Zanzibar keshokutwa Jumamosi (Novemba 13), ikiwa ni sehemu ya kujiwinda na muendelezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ambayo imesimama kupisha michezo ya kuwaniwa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022.

Baadhi ya wachezaji wa Azam FC ambao hawakuitwa kwenye vikosi vya timu zao za taifa, watacheza mchezo huo wa kirafiki ukaotapigwa Uwanja wa Azam Complex, ili kumuwezesha Kocha George Lwandamina na Benchi lake la ufundi kutambua mapungufu kabla ya kurejea kwa Ligi Kuu mwishoni mwa juma lijalo.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Azam FC Zakaria Thabit, ‘Zakazakazi’ ameweka wazi kuwa mpango mkubwa kwa msimu wa 2021/22 ni kufanya vizuri kwenye michezo ya kikosi chao na kupata alama tatu muhimu.

“Malengo yetu makubwa ni kufanya vizuri kwenye michezo ya kikosi chetu na kupata matokeo chanya hivyo mashabiki waendelee kuwa pamoja nasi ni mwendo wa kimyakimya,”

Azam FC tayari imeshacheza michezo mitano ya Ligi Kuu msimu huu 2021/22 na kukusanya alama 7 zinazoiweka nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi, huku safu yake ya ushambuliaji ikitupia mabao manne hadi sasa.

Sanjay tumaini jipya kwa wasanii wa filamu Tanzania
Zahera: Hautakua mchezo rahisi