Serikali imesema kuwepo kwa uwekezaji unaoendelea kufanyika kwenye Bandari ya Tanga hivi sasa kutasaidia kuongeza tija ya kiuchumi hasa katika kuelekea kwenye ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi linaloendelea na maandalizi ya ujenzi wake hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa jijini Tanga na mkuu wa mkoa huo, Adam Malima mara baada ya kupokea vifaa maalum vitakavyorahisisha utendaji kazi bandarini hapo ikiwemo upakuaji wa shehena.
Malima amesema ujenzi huo wa gati utakua mkombozi wa ongezeko la uchumi pamoja na fursa za ajira kwa wakazi wa Tanga na Watanzania wote kwa ujumla.
Ujenzi wa gati kwa awamu ya kwanza unatarajia kukamilika mwezi April 2022, kabla ya ule wa uongezwaji kina unaotarajiwa kukamilika Novemba 2022, huku serikali ikiwa imetoa zaidi ya shilingi milioni 450 kwa ajili ya ujenzi wa bandari hiyo.