Rais wa zamani wa Afrika Kusini FW de Klerk, lakini pia ni mzungu wa mwisho kuiongoza nchi hiyo kati ya Septemba 1989 na Mei 1994, amefariki dunia leo Novemba 11, 2021 nyumbani kwake Fresnaye Cape Town akiwa na umri wa miaka 85.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na msemaji wa familia zinasema kuwa Rais huyo wa zamani Klerk aligundulika kuwa na saratani inayoathiri utando wa mapafu mwezi Juni mwaka huu.

Aidha Klerk alikuwa mstari wa mbele katika kipindi cha mpito cha Afrika Kusini kuelekea demokrasia, ambapo mwaka 1990 alitangaza kumwachilia huru kiongozi aliyepinga ubaguzi wa rangi Nelson Mandela, na kusababisha kura za vyama vingi mwaka 1994.

FW de Klerk alichukua nafasi ya PW Botha kama mkuu wa Chama cha National Party mnamo Februari 1989 na mwaka uliofuata akatangaza kuwa anaondoa marufuku ya vyama vilivyojumuisha chama cha Mandela cha African National Congress (ANC).

Vitendo vyake vilisaidia kukomesha enzi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini, na akawa mmoja wa manaibu marais wawili baada ya uchaguzi wa vyama vingi mwaka 1994 ambao ulishuhudia Bw Mandela akiwa Rais.

Yeye na Mandela walishinda kwa pamoja Tuzo ya Amani ya Nobel mnamo 1993.

Fursa za ajira Tanga
Waziri wa ulinzi afutwa kazi Msumbiji