Jenerali mwandamizi aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi hivi karibuni nchini Sudan, Abdel-Fattah Burhan, amejiteua tena kuongoza baraza tawala la mpito, ikiwa ni hatua inayoashiria nia yake ya kuimarisha udhibiti madarakani.
Miongoni mwa walioteuliwa ni watawala waliokuwa kwenye baraza lililopita, ikiwa ni pamoja na Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, ambaye ni mshirika wa karibu wa Burhan aliyetajwa kuwa makamu wa rais, pamoja na majenerali wengine watatu waliorejeshwa.
Viongozi watatu wa makundi ya waasi pia wamejumuishwa kwenye baraza hilo na wawakilishi watano kutoka upande wa kiraia.
Licha ya ahadi zinazotolewa kila mara na watawala wa kijeshi kwamba watarejesha mamlaka kwa serikali ya kiraia, tangu mapinduzi ya Oktoba 25, ambayo yalifuatiwa na maandamano ya wanaounga mkono demokrasia wanaoshinikiza kurejeshwa kwa utawala huo wa kiraia.