Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limetoa onyo kali kuhusu madhara ya kutokujali chanjo wakati Umoja wa Ulaya ukitoa pendekezo la kuanzishwa chanjo ya lazima.

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kimataifa, kuna mchanganyiko mbaya wa idadi ndogo ya upokeaji chanjo, na idadi ndogo kabisa ya upimaji hali ambayo inachochea kuzaliana na kuongezeka kwa virusi.

Amesema lazima ulimwengu utumie zana ambazo tayari zipo ili kuzuia maambukizi na kuokoa maisha kutokana na kirusi cha Delta.

Na kwa kufanya hivyo, pia tutazuia maambukizi na kuokoa maisha kutokana na kiruso cha Omicron.

WHO imesema huenda ikachukua wiki kadhaa kubaini kama kirusi cha Omicron kinaambukiza zaidi au la, na kama kinasababisha ugonjwa mkali.

Aidha kujua jinsi matibabu na chanjo za sasa zinavyofanya kazi dhidi ya kirusi hicho.

Franco Pablo: Hatukucheza vizuri
Kocha Morocco kupoteza ajira leo?