Kampeni ya usafi iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla imeendelea kuungwa mkono na Wadau mbalimbali ambapo leo kampuni ya GNM Cargo imetoa msaada wa Vifaa vya Usafi ikiwemo Vifaa vya kuhifadhi Usafi Kama sehemu ya kuunga mkono Usafi.

Akipokea Vifaa hivyo RC Makalla amesema ni lazima mandhari ya Jiji la Dar es salaam iwe katika Hali ya Usafi na kupendeza sababu ndio lango la wageni kutoka kila Kona ya Dunia na ndio kitovu Cha Biashara.

Aidha RC Makalla ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa Kampeni ya usafi Disemba 04 kwa kufanya Usafi wa pamoja ambapo Kimkoa Kampeni hiyo itazinduliwa Kata ya Kivukoni.

 Aidha RC Makalla ameishukuru kampuni hiyo kwa kuunga mkono kampeni hiyo na kutoa wito kwa wengine kujitokeza.

Kwa upande wake Meneja masoko wa kampuni ya GNM CARGO, Amin Wille Mahava amesema kampuni hiyo itaendelea kutoa ushirikiano kwa RC kwa kutoa vifaa kila mwezi.

Aliyeuza senene kwenye ndege kufikishwa Mahakamani
RC Makalla atoa maagizo TMDA