Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza hali ya tahadhari katika mji ya Kentucky nchini humo, baada ya kukumbwa na mfululizo wa vimbunga vilivyosababisha vifo vya watu sitini huku wengine wengi wakiwa hawajulikani walipo.
Vikosi vya uokoaji vimekuwa vikiendelea na zoezi la kuwanasua watu walionasa kwenye vifusi vya majengo yaliyobomolewa na vimbunga hivyo, kwani watu wengi inasemekana bado wamenasa kwenye vifusi hivyo.
Biden amesema vimbunga hivyo ni vibaya kuliko vyote vilivyowahi kuikumba Marekani katika siku za hivi karibuni.
Habari zaidi kutoka nchini Marekani zinasema watu 70 waliokuwa katika kiwanda kimoja cha mishumaa wanahofiwa kufa, kwani kiwanda hicho kimeharibiwa kabisa.