Menaja wa Arsenal, Mikel Arteta alimuacha Nahodha na Mshambuliaji wake Pierre-Emerick Aubameyang kwenye mchezo wa Ligi Kuu England juzi Jumamosi (Desemba 11) dhidi ya Southampton kutokana na “kuvunja sheria za kinidhamu.”

Akizungumza kabla ya mchezo huo, Arteta alisema: “(Aubameyang hatacheza) kwa sababu ya kuvunja sheria za kinidhamu.”

“Nafikiri tumekuwa wazi kabisa kuhusu nidhamu ya timu na lazima kila mchezaji anatakiwa kufuata sheria.”

Alipoulizwa kama hiyo itakuwa adhabu ya muda mrefu, Arteta aliongeza: “Inaanza leo (juzi).

“Pengine sio hali ya rahisi, au hali ambayo tunaitaka kutoka kwa nahodha wa klabu yetu.”

Aubameyang pia alicheza kwenye mchezo wa Machi mwaka huu wakishinda dhidi ya wapinzani wao wa London, Tottenham baada ya kuchelewa kujiunga na timu hiyo siku ya mchezo.

Arsenal katika mchezo wa juzi iliibuka na ushindi mtamu wa mabao 3-0 na kujivuta hadi nafasi ya sita kwenye msimamo ikiwa na pointi 26 baada ya kushuka dimbani mara 16.

Biden atangaza hali ya tahadhari
Lwandamina afunguka kufukuzwa kazi Azam FC