Kocha George Lwandamina amethibitisha kupokea taarifa za kutimuliwa kazi na Uongozi wa Azam FC, kama ilivyoelezwa mapema hii leo kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania.

Lwandamina ameondolewa kazini sambmaba na Msaidizi wake Vivier Bahati, kufuatia kikosi cha klabu hiyo kuanza vibaya Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu 2021/22.

Lwandamina amesema: “Nimepokea taarifa hiyo lakini naenda kuonana na viongozi wa klabu, ni maisha yetu ya mpira.”

Kocha huyo mwezi uliopita alisaini mkataba mpya wa mwaka mmoja lakini mabosi wake wameamua kuuvunja mkataba huo, kwa kutazama maslahi ya kikosi chao.

Azam FC mpaka sasa inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bra ikiwa na alama 11, ikishinda michezo mitatu, sare mbili na kupoteza michezo mitatu.

Arteta: Aubameyang hana nidhamu
Salum Mayanga akabidhiwa Mtibwa Sugar