Beki wa kati Maafande wa JKT Tanzania, Salum Athuman ‘Stopper’ amesema kikosi chao kitawapa heshima ya kutosha Mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ Simba SC, kwenye mchezo wa leo Jumanne (Desemba 14).

Simba SC itakuwa mwenyeji wa mchezo huo wa mzunguuko wa tatu wa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, saa moja usiku.

Salum amesema wanaamini Simba SC ina kikosi kizuri na ndio Mabingwa watetezi, hivyo hawana budi kuwapa heshima hiyo, lakini watapambana wakati wote ili kupata matokeo yatakayowavusha na kwenda hatua inayofuata.

“Tunacheza na timu kubwa Simba, tutawapa heshima zote tutacheza kwa nidhamu pia tutaangalia udaifu wao na kuangalia namna ya kushinda.” amesema Salum

Simba SC ilitetea Ubingwa wa ‘ASFC’ msimu wa 2020-21 kwa kuifunga Young Africans bao 1-0 katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Msimu wa 2019-20 Simba SC ilitwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa kuifunga Namungo FC mabao 2-1, katika Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Tanzania Prisons wazindua uzi mpya
Koffi Olomide ahukumiwa miezi 18 jela