Inaelezwa kuwa Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Zambia, Clatous Chotta Chama amefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na klabu ya RS Berkane ya Morocco.

Chama alisajiliwa na RS Berkane kwa mkataba wa miaka mitatu mwanzoni mwa msimu huu, akitokeza kwa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC.

Taarifa zinaeleza kuwa Mkataba wa Chama na RS Berkane utakoma rasmi Januari 2022, na atakua huru kujiunga na klabu yoyote ndani na nje ya Afrika, huku Simba SC ikipewa kipaumbele cha kumsajili.

Sababu kubwa ya Chama kusitisha mkataba wake klabuni hapo ni kushindwa kukabiliana na hali ya hewa na chakula nchini humo.

Wakati Chama akifanya maamuzi ya kubunja mkataba wake, Usajili wa Dirisha Dogo kwa Tanzania linafunguliwa rasmi kesho Jumatano (Desemba 15).

Songne kuleta mshambuliaji Young Africans
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Disemba 14, 2021