Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amevunja ukimya kuhusu kinachomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akisema kuwa demokrasia ni kuheshimu sheria.

Amesema hayo leo Desemba 15, 2021 wakati akifungua mkutano wa wadau kujadili demokrasia ya vyama vingi, Rais Samia amesema ni muhimu kuzingatia sheria za nchi.

Rais Samia amesema hayo wakati akijibu ombi la Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Zitto Kabwe aliyemuomba kusaida kuachiwa kwa Mbowe ambaye pamoja na wenzake watatu wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 16/2021 yenye mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili vitendo vya kigaidi, inayoendelea katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

“Nataka nijibu lile ombi la mwanangu, iko hivi demokrasia ni kuheshimu sheria, unapoheshimu sheria ndipo demokrasia inapokua, lakini pia ndipo inapoleta heshima”amesema Rais Samia

“Heshima ya mtu inakuja unapoheshimu sheria za nchi, unapovunja sheria za nchi heshima yako haitaheshimiwa, Serikali haitakuheshimu lakini lazima ujue kwamba unapotumia uhuru wako mwisho wa uhuru wako inaanza heshima ya mtu mwingine,”.

”Isingekuwa uvunjifu wa sheria leo isingemlazimu Zitto kuomba hapa kwamba yule mwenzetu muachie lakini unapovunja sheria unajivunjia heshima

“Naomba tufanye kazi kwa kuheshimu sheria, waswahili wanasema mtaka nyingi nasaba hupata mingi misiba, ingawa kusameheana nako kupo,”

Rais Samia akemea wanasiasa kusema uongo
Katwila: Hatuiogopi Young Africans, tunaiheshimu