Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifello Sichalwe amesema serikali imefatilia dalili za kukohoa, mafua, maumivu ya mwili na kuchoka, na kubaini kweli kuna ongezeko la Wananchi kupata dalili hizo na ameeleza kuwa hiyo ni hali ya hewa kama ambavyo iliweza kushuhudiwa kwa miaka mingine iliyopit
“Hata hivyo, hii huwa ni hali ya kawaida kila mwaka (seasonal influenza) ambayo huchangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa kama ambavyo iliweza kushuhudiwa kwa miaka mingine iliyopita, hata hivyo, Wizara na taasisi zake tunaendelea kufuatilia kwa karibu viashiria vya mwenendo wa hali hii” alisema dkt Sichalwe.

Aidha, Wizara inashauri kuwa wananchi wenye dalili hizi za kukohoa, mafua, maumivu ya mwili na kuchoka watoe taarifa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili wafanyiwe uchunguzi wa kitaalamu na wapatiwe matibabu stahiki.

“Pamoja na hali hii ya mwenendo wa mafua ya kawaida, vilevile Wizara inaendelea kukumbusha na kutoa tahadhari kwa kila Mtu kuendelea kuchukua hatua zote muhimu za kujikinga na janga la UVIKO-19 ikiwa ni pamoja kuepuka misongamano isiyokuwa ya lazima, kunawa mikono, kuvaa barakoa na kuhakikisha kuwa kila Mtu anapata dozi kamili ya chanjo”.


“Wito kwa wananchi kutoa taarifa za tetesi za viashiria vya magonjwa ya mlipuko kutoka katika jamii kupitia namba ya simu 199 bila malipo yoyote.” alisema Dkt. Sichalwe.

Katika kuhakikisha Umma unapata taarifa za mwenendo wa mafua katika kipindi hiki, Wizara imeelekeza taasisi za utafiti kitaifa kama NIMR, Vyuo vikuu na watalaam wote kuendelea kutoa takwimu na elimu kutokana na ufuatiliaji wa kisayansi [Survellience] ambao watakuwa wakifanya kutokana na visa vya mafua nchini.

Katika hatua nyingine ameendelea kuwakumbusha wanananchi kuendelea kuchukua hatua katika kipindi hiki cha mwisho mwa mwaka.

“Napenda kuwakumbusha kuwa, ugonjwa wa UVIKO 19 bado upo na huenda maambukizi ya ugonjwa huu yakaongezeka hasa tunapoelekea mwisho wa mwaka unaohusisha kipindi cha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka hivyo, vema tuzingatie kuchukua tahadhari.”

Timu za Bunge la Tanzania zaibuka kidedea kombe la Jumuiya ya Afrika mashariki
Askari aliyesifia gongo afukuzwa kazi