Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 18, 2021 amezipokea timu za michezo mbalimbali za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika viwanja vya Bunge, Jijini Dodoma.

Timu hizo zimefanikiwa kushinda makombe Saba kwa michezo mbalimbali katika mashindano ya 11 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki yaliyofanyika Jijini Arusha.

Akizungumza baada ya kupokea timu hiyo Waziri Mkuu amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezipongeza timu zote zilizotwaa makombe katika mashindano hayo.

Pia Waziri Mkuu amempongeza spika wa Bunge Job Ndugai kwa maandalizi mazuri ya timu hizo ambazo zimewezesha kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Timu ya Bunge imeshinda makombe kwenye michezo ya mpira wa miguu, pete, wavu kwa wanawake na wanaume, kikapu kwa wanawake na wanaume na mchezo wa kuvuta kamba wanaume

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Disemba 19, 2021
Dkt Sichalwe:Ni mafua ya Kipindi "seasonal Influenza"