Takriban watu 75 wameripotiwa kupoteza maisha katika kimbunga kikali zaidi kuwahi kuikumba Ufilipino mwaka huu, huku juhudi za kupeleka maji na chakula katika visiwa vilivyoharibiwa zikiongezeka.
Zaidi ya watu 300,000 wamekimbia makaazi yao na maeneo ya ufukweni wakati kimbunga Rai kilipopiga na kuharibu maeneo ya kusini na kati ya visiwa hivyo.
Kimbunga hicho kimeka mawasiliano na umeme katika maeneo mengi, pamoja na kuezua mapaa na kuangusha nguzo za umeme ziliyojengwa kwa saruji.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook gavana wa mji wa kitalii wa Bohol, Arthur Yap, amesema mameya kwenye kisiwa hicho wameripoti vifo 49 katika miji yao hadi kufikia sasa idadi jumla ya vifo iliyoripotiwa imefikia 75.
Yap ameongeza kuwa watu 10 bado hawajulikani walipo na wengine 13 wamejeruhiwa kutokana na dhoruba hiyo.