Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Ummy Mwalimu amempa mamlaka Katibu Tawala za Mkoa wa Singida kusaini malipo ya mafundi wanaojenga Kituo cha Afua Ilunda katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.

Waziri Ummy, ametoa maamuzi hayo wakati akikagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo na kufika kwenye Kituo cha Afya Ilunda ambacho kiko nyuma kwenye ujenzi kwa sababu ya mivutano ya Baraza la Madiwani katika Halmashauri hiyo.

‘Nimeambiwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hii anakataaa kusaini mikataba ya ujenzi sababu tu hajaafiki kituo hiki kijengwe Ilunda na hata kazi hii kuchelewa kuanza ni kwa sababu ya mivutano hiyo mpaka TAMISEMI kuingilia kati na kutoa maelekezo’

Liverpool yapelekwa London, Chelsea kuivaa Spurs
Luis Miquissone atwaa CAF Super Cup