Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amethibitisha kifo cha mshindi wa Nobel na miongoni mwa watu muhimu kumaliza ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, Askofu Emeritus Desmond Tutu
Desmond Tutu amefariki katika umri wa miaka 90 kwa sababu za kiafya ambazo ni kusumbiliwa na Saratani ya Kibofu
Tutu aligundulika kuwa na saratani ya kibofu mwishoni mwa miaka 1990 na amelazwa mara kadhaa kwa maradhi yanayohusiana na matibabu ya saratani hiyo
“Kifo chake kimefungua ukurasa mpya wa majonzi na kuongeza idadi ya mashujaa waliofariki walioipigania nchi yetu na Afrika kwa ujumla na tutaendelea kumkumbuka” amesema Rais Cyril Ramaphosa.
Taarifa za familia ya Tutu zinamuelezea kwa sentensi moja kama “mtu alietumia matatizo yake kama njia ya kufundisha jamii jinsi ya kujali shida na matatizo ya wengine”
“Alitaka Dunia ifahamu kuwa anasumbuliwa na Kansa ya tezi dume na mtu akiwahi kugundulika anatibiwa na kupona.”
Tutu ndiye alieanzisha msemo wa “Rainbow Nation” akimaanisha taifa lenye upinde wa rangi ya mvua wakati ambao Hayati Nelson Mandela akiwa Raisi wa Kwanza mweusi nchini Afrika Kusini.
Alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 1984 kwa kuongoza kampeni ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini