Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Otile Brown ameingia kwenye rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa Kenya kupata idadi ya wafuasi (Subscribers) milioni 1 kwenye mtandao wa YouTube.

Otile Brown ambaye alijiunga na mtandao huo Aprili 20, 2016, hadi sasa amepata watazamaji zaidi ya 251,743,575 kwenye chaneli yake.

Otile anashika namba moja akifuatiwa kwa ukaribu na Bahati ambaye ana wafuasi (Subscribers) 902K na zaidi ya watazamaji 151,289,133 tangu kujiunga na mtandao huo mnamo Agosti 7, 2012.

Kwa upande wa Sauti Sol mpaka sasa wamepata Subscribers 856K na kutazamwa na zaidi ya watu 220,181,008 tangu kujiunga na mtandao huo mnamo Aprili 9, 2012.

Wengine ni King Kaka (Subscribes 360K), Khaligraph Jones (Subscribers 538K), Nyashinski (473K), Mukami (439K), pamoja na Nadia Femi One (225K).


Kwa mujibu wa maelezo kutoka youtube, inaelezwa kuwa Wafuatiliaji (Subscribers) ni muhimu sana kwa mafanikio ya mtumiaji kwa kuwa hutumia muda mwingi kufuatilia kuliko watazamaji ambao hawa-subscribe.

TANESCO kufanya matengezo ya dharura
Mrembo aliejitabiria kifo chake aaga dunia