Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Italia na Klabu ya Juventus, Federico Chiesa amemaliza msimu wa 2021/22, baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti Jumapili (Januari 23).

Chiesa aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Italia ‘Serie A’ dhidi ya AS Roma, ambapo Juventus ilichomoza na ushindi wa mabao 4-3 majuma mawili yaliyopita.

Upasuaji aliofanyiwa Chiesa hautamuwezesha kuonekana tena Uwanjani katika kipindi cha msimu wa 2021/22 kilichosalia, na anatarajiwa kurejea dimbani mwanzoni mwa msimu ujao.

“Mchana wa leo (Jumapili), Federico Chiesa alifanyiwa upasuaji wa goti lake la kushoto na atakuwa nje kwa muda wa miezi saba.” imeeleza taarifa ya Juventus FC

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 anaondolewa katika mipango ya kikosi cha Timu ya Taifa ya Italia ambacho kitacheza mchezo wa mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia 2022.

Mabingwa hao wa Ulaya watamenyana na Macedonia Kaskazini katika mwezi Machi na kisha watakutana na Uturuki au Ureno kuwania kufuzu kwenda Qatar.

Chico Ushindi aongeza jeuri Young Afrcans
Bao lamtia wazimu Sergio Ramos